John 12:2-3

2 aWakaandaa karamu kwa heshima ya Isa. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Isa. 3 bKisha Maria akachukua chupa ya painti moja
Painti moja ni kama nusu lita.
yenye manukato ya nardo
Nardo ni aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri.
safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Isa na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.

Copyright information for SwhKC